Friday, July 5, 2013
Je wamjua Simba-mangu?
Simba-mangu(Caracal) ni mnyama mzito mwenye uzito zaidi kati ya jamii yake ya mapaka,Simba mangu dume anaweza kuwa na uzito kati ya kilo 15 mpaka 18 na majike uzito wao ni kati ya Kilo 13 na kuendelea........
Miguu ya nyuma ya Simba mangu ni mirefu kuliko ya mbele ya mbele...Simba mangu ana uwezo wa kuona zaidi usiku na hata mchana tofauti na wanyama wengine wanaoweza kuona vizuri zaidi usiku au wanao-ona vizuri mchana lakini usiku hawaoni vizuri,Simba-mangu yeye usiku na mchana anaona vizuri tu...
Simba mangu huwa wana-aibu na niwapandaji wazuri wa miti.
Hupenda Kula nini?
Simba-mangu hupendelea kula vitu kama vile,Pimbi mawe(Hyrax),Mbuzi mawe(Klipsringer),panya,Sungura,Mijusi,na Ndege...na wanauwezo wa kuruka juu hadi futi 11 sawa na mita 3-4....
Hukaa na mimba mda GANI?
Huwachukua takribani siku 62-82 sawa na miezi miwili na zaidi na watoto kati ya 2-4 huzaliwa na wanaweza kuishi hadi miaka 12...
MAADUI:
Wanyama wakubwa kunzidi yeye mfano,chui,simba n.k
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment