Punda milia dume anaweza akawa na uzito kati ya kilo 380 na jike kati ya 320 na wanapendelea kukaa sehemu zenye nyasi fupi na wanapendelea sana kuishi katika makundi na wanapenda sana kushirikiana makazi na nyumbu.....
Hupendelea kula zaidi nyasi fupi na mara nyingine hula vichaka vidogo vidogo na majani ya miti midogomidogo.....
Pundamilia wote wana mistari lakini kamwe mistari yao haifanani,na hii inawasaidia watoto wao kuwatofautisha wazazi ama kuwatambua wazazi wao kwa kuangalia mistari hiyo na pia mistari hii hii ya punda milia ni muhimu pia kwao kwa ajili ya ulinzi wao kwa sababu ni aina ya fumbo fulani ama muundo wenye nia ya kuwachanganya adui zao pindi wanapowindwa na wanyama walao nyama kama vile chui,simba,fisi,mbwa mwitu n.k kwa kuwadanganya macho maadui zao....
Hupendelea sana kukaa mkao wa mashariki magharibi au kaskazini kusini yaani,mmoja huelekeza kichwa chake upande wa mashariki na mwingine upande wa magharibi au kaskazini kusini kwa ajili ya usalama wao zaidi ili adui anapotokea upande wa mashariki,ambae amegeukia mashariki anamtaarifu ambaye amegeukia magharibi au aliyegeukia kaskazini anamtaarifu aliyegeukia kusini...Hii inawasaidia sana kwa ajili ya ulinzi wao binafsi.....
Pundamilia hubeba mimba kati ya miezi 12 mpaka 13 na mtoto anayezaliwa ni mmoja tu na huishi kati ya miaka 10 na 11
Adui mkubwa wa Pundamilia ni binadamu,Simba,Mbwa-mwitu na Fisi.....
Tazama jinsi walivyokaa kwa ajili ya kuboresha usalama wao,mashariki magharibi.........
No comments:
Post a Comment