Mbwa ni kiumbe anayefugwa nyumbani na kuzoeleka na watu mbali-mbali...Mbwa huaminika kwa ulinzi wa majumbani mwetu na kutufanya angalao tuishi kwa raha japo kidogo....
Kuna zaidi ya jamii takribani 30 za mbwa katika familia hii....
Hebu tumzungumzie kidogo Mbwa pori {African Hunting Dog}..kwa mbwa mwitu ambaye ameshakuwa anakadiriwa kuwa na meno 42,hawa wanyama hupatikana karibia kote kusini mwa sahara isipokuwa maeneo yenye msitu...Mbwa mwitu wanapenda kuishi kwa makundi makundi kati ya jozi 2 mpaka 3...
Mbwa mwitu huhama sehemu moja kwenda sehemu nyingine zaidi ya kilometa 10.Ni wanyama wenye speed kali sana na wanapenda kuwinda kwa ushirikiano mkubwa ambapo Mbwa mwitu wenye umri wa kati wanapewa jukumu la kuwaangalia watoto na kuwaacha Mbwa Mwitu wakubwa kwenda kuwinda na HUWALISHA WATOTO WAO KWA KUWATAPIKIA kwambaaaa wazazi wao hukwenda kuwinda na kula mpaka washibe na wakirudi toka mawindoni huwatapikia watoto wao chakula walichokula....
Mbwa mwitu wanakadiriwa kuwa na uzito kati ya kilo 25- 35 na wanauwezo wa kuona zaidi usiku kuliko mchana na hubeba mimba kwa mda wa miezi 2 na kwa kawaida watoto wanaozaliwa ni kati ya 6-10 kwa wakati mmoja na wakati mwingine hata watoto 12 huzaliwa na wanauwezo wa kuishi kati ya miaka 10 mpaka 12 na kama ilivyo kwa viumbe wengine,Mbwa mwitu nao wana maadui wao wakubwa ambao ni wewe na wanyamawengine wakubwa walao nyama kama vile Simba,chui,duma n.k na pia tunaweza kusema kuwa adui mwingine wa Mbwa mwitu ni Mvua kwani Mbwa mwitu huwahifadhi watoto wao kwenye mashimo waliochimba ambapo endapo mvua ikinyesha husababisha watoto wao kufa kwa ya maji ambayo yanaingia kwenye mapango yao na kumomonyoa kuta za mapango yao.......
No comments:
Post a Comment