Monday, August 5, 2013

Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya huko Zimbabwe

Lile vugu vugu la Watanzania kuendelea kuhusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya linazidi kukua siku hadi siku baada ya Mtanzania Jackline Moleli kukamatwa na kilo 15 za madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege wa Harare huko nchini Zimbabwe ...........



Monday, July 29, 2013

Kamishna Kova awaasa wananchi kufichua wezi majumbani kwao...

Kutokana na uhalifu ulioibuka tena wa raia kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana na wizi wa kutumia piki piki hasa aina ya Boxer,kamishna wa kanda maalumu ya Dar-es-salaam Suleiman Kova amewaasa wananchi kuwafichua wezi majumbani mwao ili waweze kuchukuliwa hatua na kusisitiza kuwa endapo itabainika umemficha mhalifu au unakaa na mhalifu bila kuripoti kituo cha polisi na wewe utachukuiliwa hatua kama mhalifu....
Kuwa mzalendo wa Inchi yako

Saturday, July 27, 2013

Tazama picha za kufungia siku

Hahahahaha,hata wanyama nao wana-mbwembwe zao...Ona mwenyeewe

Mazee nina njaa balaaa,yaani naona mapichapicha tu,naona kama vile mbingu hii hapaaa....kama kuna mtu ana buku anitoe basi....

Si lazima nifundishwe kutembea bhana,me mwenyewe naweza....

 Kuna fresh hapo bhana

Huu ndiyo ulaji wa kidigital
 

Ukuti ukuti,wa meme....wa meme....kama hukumbuki haka kamchezo polee

 Mmmm,asije jua maana haambiwi maana,tehe tehe tehe......

Duuu,halafu ningesahau,mama weeeh,duuh bora nimekumbuka mapema.....

Chezea weekend wewe,ninamausingizi balaaaa
 
 Hehe heiya,umepotea sana shosti tokea uolewe ndiyo bhasi tena,jamani huyo mumeo anakukeep busy eehh,mbona majanga??vipi kibati kimefikia wapi mzunguko wake,?au mwenzangu siku hizi ni mambo ya vibubu??????

 Utanieleza fresh kwamba aliyekutuma uwaambie watu kuwa me m-mbwa mwitu nani...mbona utajibeba leo?

 Ufupi thio hoja bana,lazima kieleweke........

Then tukutane jioni kwenye Futari

Utani mwingine bwana.......cheka upate afya...

Daktari mmoja alipomaliza kumzalisha mama mmoko katika hospitali moja hapa bongo akawa anamtania na kumwambia"Hongera umezaa jambe"Ghafla mama wa watu akazimia...Daktari "heee makubwa"
Mama kuzinduka akakutana uso kwa uso na daktari,daktari ikabidi amuulize haya kulikoni ukazimia?mama akadakia " yaani nibebe mimba kwa miezi 9 halafu nizae jembe nani kakuambia kuwa mume wangu ni mkulima?"daktari ahahahahahahahahaha,sikumaanisha hivyo bwana,nilimaanisha kuwa umezaa mtoto wa kiume....mama aaaaahahaha tengua kauli....

Friday, July 26, 2013

The Master of Camouflage....

Camouflage is the use of any combination of materials, coloration or illumination for concealment, either by making animals or objects hard to see....Leopard is the One,now
Leopard(Chui) is the fourth largest cat after the tiger,lion and the American Jaguar..Leopard occur in the different areas all over Africa and in South Asia except in the desert...Males are lager than females and in males scrotum can be easily seen hanging below the anus....
A leopard is a solitary animal and is more nocturnal than lion and leopard spend the day time resting and hidden in thick bush,rocks,caves,burrow or sleep on branch of tree and kills are taken up the tree to avoid food competition with other animals and feeds on gazelles,impala,warthog,monkey,birds,hares,rodents,baboon and even dogs

Leopard is solitary or in pair during mating season and Gestation Period is about 3 month and the litter size is 1-3 cubs but it is very unlikely that all the cubs would survive in their lifetime because the mortality rate in the young are very high and leopard live up to 15 years...

The best place where one is likely to encounter a leopard  is Lobo and Seronera valley in Serengeti National Park in Tanzania...

Thursday, July 25, 2013

Wazo la kufungia siku.........

"Hata kufuli linafunga lakini halifuturu"

Jioni njema...

Je waijua kazi ya mistari katika Pundamilia?


Pundamilia hupatikana karibia kila hifadhi hapa Tanzania,Dume huwa ni mkubwa kuliko jike na dume ana meno chonge(Canine)kwa ajili ya kupambana na maadui....
Punda milia dume anaweza akawa na uzito kati ya kilo 380 na jike kati ya 320 na wanapendelea kukaa sehemu zenye nyasi fupi na wanapendelea sana kuishi katika makundi na wanapenda sana kushirikiana makazi na nyumbu.....
Hupendelea kula zaidi nyasi fupi na mara nyingine hula vichaka vidogo vidogo na majani ya miti midogomidogo.....
Pundamilia wote wana mistari lakini kamwe mistari yao haifanani,na hii inawasaidia watoto wao kuwatofautisha wazazi ama kuwatambua wazazi wao kwa kuangalia mistari hiyo na pia mistari hii hii ya punda milia ni muhimu pia kwao kwa ajili ya ulinzi wao kwa sababu ni aina ya fumbo fulani ama muundo wenye nia ya kuwachanganya adui zao pindi wanapowindwa na wanyama walao nyama kama vile chui,simba,fisi,mbwa mwitu n.k kwa kuwadanganya macho maadui zao....
Hupendelea sana kukaa mkao wa mashariki magharibi au kaskazini kusini yaani,mmoja huelekeza kichwa chake upande wa mashariki  na mwingine upande wa magharibi au kaskazini kusini kwa ajili ya usalama wao zaidi ili adui anapotokea upande wa mashariki,ambae amegeukia mashariki anamtaarifu ambaye amegeukia magharibi au aliyegeukia kaskazini anamtaarifu aliyegeukia kusini...Hii inawasaidia sana kwa ajili ya ulinzi wao binafsi.....
Pundamilia hubeba mimba kati ya miezi 12 mpaka 13 na mtoto anayezaliwa ni mmoja tu na huishi kati ya miaka 10 na 11
Adui mkubwa wa Pundamilia ni binadamu,Simba,Mbwa-mwitu na Fisi.....

Tazama jinsi walivyokaa kwa ajili ya kuboresha usalama wao,mashariki magharibi.........

Wednesday, July 24, 2013

Ama kweli macho hayana pazia.....

Vijana wawili nusura watumbukie darajani kwa kumkodolea macho mrembo mmoja aliyekuwa anavuka barabara...."Mtakufa nyie"alisikika akisema dada huyo na kuondoka katika eneo lile....duuh ujana maji ya moto.....watazame  kwa mbali.!!!!!!!!
Mbona majangaaa!!!

Je wamjua mnyama asiyependa usumbufu?


Duma ni mnyama mwenye sura nzuri katika jamii ya mapaka wote tukimlinganisha na chui,simba,simba mangu,mondo,paka pori na wengineo....Mnyama huyu huwa na uwezo wa kuona zaidi wakati wa mchamna kuliko usiku na ni mnyama mwenye kasi zaidi aridhini,anakimbia kwa kasi ya 110 k.m.p ambapo madume ni makubwa zaidi kuliko majike na wanakadiriwa kuwa na uzito kati ya kilo 60-70......Duma{Cheetah}hupendelea kula wanyama wadogo wadogo kama vile swala tomi{Thomson Gazzele}sungura pori na hata ndege mda mwingine na katika utafutaji wake wa chakula hupendelea kukaa juu ya kichuguu na kuchagua mnyama anayempenda na kuanza kumshughulikia kwa kumkimbiza kwa kasi ila kuna wakati mnyama anayewindwa humzidi mbio Duma na duma hukata tamaa na kumwacha mnyama wake aliyemchagua na hii hutokea mara chache pale ambapo duma anaposhindwa kukadiria umbali halishi wa mnyama aliyemchagua kwa mlo wake wa siku....
.Duma ni mnyama asiye penda usumbufu awindapo kwani akiwa anawinda halafu kikatokea kitu kika-mbuguzi huwa anaacha kuwinda na atakaa na njaa mpaka siku inayofuata bila kula chochote na pia ni mnyama ambaye hapendi vurugu pindi anapokula,mfano akiwa anakula halafu wanyama mwengine kwa mfano fisi,tai mizoga,simba na wengineo wakimuingilia katika mlo wake huacha kula na kuondoka tunaweza sema ni Peacefull Animal...
Huzaa watoto kati ya wa 2 hadi wa 4 na ubebaji wao wa mimba ni kati ya ya miezi mi 3 na mi 4 na huweza kuishi mpaka miaka10 na adui yake mkubwa ni Binadamu

        

Tejaaaaaaaaaaaaaa...hhahahahaha

Teja alikuwa anavuta unga akasikia sauti ya ajabu,teja akauliza "NANI WEWE?"
Akajibiwa ni mimi Israeli mtoa roho teja Akajibu daah man umenistua kishenzi,mi nilizani polisi bhana kumbe ni wewe jembe

Friday, July 19, 2013

Mhe.January Makamba Amjibu Mh.John Mnyika kuhusu sakata la KODI ya shilingi 1000 kila mwezi kwa kila line ya simu unayoimiliki

                                                              


Lile sakata la kila mmiliki wa simu kulipa shilingi 1000 kwa kila sim card anayoimiliki limeingia katika sura mpya baada ya Naibu waziri wa mawasiliano,sayansi na teknolojia Mheshimiwa January Makamba kumtaka Mbunge wa Ubungo John Mnyika kuacha 'unafiki' wa kujitetea kuhusu kodi ya laini za simu maana wote walilipitisha bungeni,Ambapo mh.January Makamba ame-Tweet hivi katika tweeter akisema.........

January Makamba @JMakamba 2h
Mnyika acha unafiki. Sote tumeshindwa kuwatetea wananchi on‪#‎SIMCardTax‬ Bungeni. Turudi Bungeni tuondoe hii kitu sio kutapatapa mitandaoni





Wananchi tusubiri tuone mwisho wake.....!!!!!!!!

Kuhusu kulipia card za simu kila mwezi,Mh. John Mnyika Afunguka...Je ni nini??Msome hapa

Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.



Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:

Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo. 
Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Ambacho sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema uongo, kwa kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu suala hili baada ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza kulishughulikia bungeni mara baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi lukuki za simu ikiwemo hii. Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba muswada huo wa sheria ya fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni ‘muswada wa majanga ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi. 

Aidha, sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa mujibu wa kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya kupinga kodi ya umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote zenye kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta ya mawasiliano bali pia kwenye sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub sector) nyeti ya mafuta. 

Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na ikalirudia kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya Serikali; ni wakina nani hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge walioingiza kodi hii? Na ni wakina nani hasa waliopigia kura ya ndio kuipitisha? 

Aidha, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba hakubaliani na suala hili na kupita kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo, ataje kwa majina hayo waliozidi nguvu serikali kinyume na matakwa yake. Amenukuliwa akisema pia kwamba anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na kwamba ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi. Ni vizuri akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa kodi hiyo katika mkutano ujao? 

Wakati Naibu Waziri akisema hayo, Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo hiyo yeye ametoa kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu za kiganjani.

Na kwa kuwa amesema kwamba Serikali inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito kwa wananchi kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi 0754/0684-765644. Aidha, ni vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa kwa majina waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake aliyosoma bungeni kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa majina waliomfanya arejeshe kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha alilowasilisha bungeni.

Nasisiza kuwa kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine mwenye mamlaka ajitokeze kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha mchakato wa muswada wa kufuta kodi hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti 2013. 

Majina ya wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika mkutano wa hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni nitatoa mrejesho kuhusu yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na kueleza hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge hao kutajwa hadharani na hatua za kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa.

Uongozi bora na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi. Twende kazi.

John Mnyika (Mb)
19 Julai 2013

Thursday, July 18, 2013

Je wamjua mnyama wa porini anayewalisha wanae kwa Kuwatapikia...???

Mbwa ni kiumbe anayefugwa nyumbani na kuzoeleka na watu mbali-mbali...Mbwa huaminika kwa ulinzi wa majumbani mwetu na kutufanya angalao tuishi kwa raha japo kidogo....
Kuna zaidi ya jamii takribani  30  za mbwa katika familia hii....

Hebu tumzungumzie kidogo Mbwa pori {African Hunting Dog}..kwa mbwa mwitu ambaye ameshakuwa anakadiriwa kuwa na meno 42,hawa wanyama hupatikana karibia kote kusini mwa sahara isipokuwa maeneo yenye msitu...Mbwa mwitu wanapenda kuishi kwa makundi makundi kati ya jozi 2 mpaka 3...
Mbwa mwitu huhama sehemu moja kwenda sehemu nyingine zaidi ya kilometa 10.Ni wanyama wenye speed kali sana na wanapenda kuwinda kwa ushirikiano mkubwa ambapo Mbwa mwitu wenye umri wa kati wanapewa jukumu la kuwaangalia watoto na kuwaacha Mbwa Mwitu wakubwa kwenda kuwinda na  HUWALISHA WATOTO WAO KWA KUWATAPIKIA kwambaaaa wazazi wao hukwenda kuwinda na kula mpaka washibe na wakirudi toka mawindoni huwatapikia watoto wao chakula walichokula....
Mbwa mwitu wanakadiriwa kuwa na uzito kati ya kilo 25- 35 na wanauwezo wa kuona zaidi usiku kuliko mchana na hubeba mimba kwa mda wa miezi 2 na kwa kawaida watoto wanaozaliwa ni kati ya 6-10 kwa wakati mmoja na wakati mwingine hata watoto 12 huzaliwa na wanauwezo wa kuishi kati ya miaka 10 mpaka 12 na kama ilivyo kwa viumbe wengine,Mbwa mwitu nao wana maadui wao wakubwa ambao ni wewe na wanyamawengine wakubwa walao nyama kama vile Simba,chui,duma n.k na pia tunaweza kusema kuwa adui mwingine wa Mbwa mwitu ni  Mvua kwani Mbwa mwitu huwahifadhi watoto wao kwenye mashimo waliochimba ambapo endapo mvua ikinyesha husababisha watoto wao kufa kwa ya maji ambayo yanaingia kwenye mapango yao na kumomonyoa kuta za mapango yao.......

Monday, July 15, 2013

Cheka kidougoooooooooo

Siku moja mkulima mmoja aliamka asubuhi kwenda kupalilia shamba lake...Njiani akakutana na SIMBA,,,,,,mkulima akaanza kupiga magoti na kufumba macho ki-uoga na kuanza kupiga sala zake za mwisho akiamini kuwa huenda anaweza akanusurika kwenye kucha za SIMBA....Alipomaliza sala akafungua macho na kushangaa kumuona SIMBA na yeye kapiga magoti huku kafumba macho...Mkulima akabaki anaduwaa...Mkulima akamuuliza simba  'KUMBE NA WEWE NI MKRISTO????'Simba akamwambia "INA-MAANA HUWA HAMSALI KABLA YA KULA????"mkulima chini,kilichoendelea pale mi nilikuta tu Jembe

Wednesday, July 10, 2013

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni....Mtazame huyu...



                                             
Amakweli tembea uone....Hii njemba ilionekana mida ya saa Nane usiku ikivinjari katikati ya jiji la Arusha maeneo ya Clock-Tower....Haikufahamika mara moja kwamba ni kichaa au ndo maandiko ya mganga wake yanatimizwa au la...Alionekana ikitembea katikati ya barabara bila kujali baridi kali au hata kugongwa na gari.....lakini cha ajabu alipotea katika mazingira ya kutatanisha na kilichoonekana ni boksi alilokuwa amelishikilia....Mtazame hapa akiwa kwenye anga zake.......
                                                                 

Tuesday, July 9, 2013

Silence Killer.....

Hii ndiyo inayowamaliza vijana wengi alimaarufu veve ambapo unakuta kijana kabugia utafikiri anakula mboga za majani bila kujali madhara yake hapo mbeleni....zindukaaaaaaaaa.....

Kwa hali hii tutaachwa kuvunjwa miguu kweli????????

Mtazame huyu jamaa aliyenaswa na kamera ya Spider akijifunza kuendesha boda-boda peke yake halafu kesho unamkuta kapakiza abiria barabarani....Je tutaponaaaaa?????
         
                                                 
majanga...

Maajabu ya Kichuguuu....

Kichuguu waweza kukiona kwa nje kuwa ni kitu cha kawaida sana lakini kina maajabu makubwa ndani yake.....Kichuguu kimeundwa kwa udongo na mabaki mabaki yamimea....
Ndani ya kichuguu kuna mgawanyo wa vyumba na mgawanyo wa majukumu mbali-mbali ndani ya kichuguu na hata nje ya kichuguu....
Kichuguu chaweza kuwa na mgawanyo wa vyumba hata zaidi ya vitatu ila vyipo vyumba ambavyo ni vyumba ambavyo ni vya muhimu sana,
Chumba cha Kwanza kinajulikana kama Royal chamber:Ndani ya hichi chumba ndipo waishipo wakuu wa kichuguu yaani MALKIA NA MFALME....Hichi chumba hutumika kama ikulu ambapo amri zote na mambo yote hupagwa hutoka ndani ya ya hichi chumba....
Chumba cha Pili kinaitwa Incubation Chamber:Hichi chumba ni kwa ajili ya kutagia tu kisha baada ya mayai kutagwa hupelekwa kwenye chumba cha Tatu kijulikanacho kama Waiting Chamber ambapo mayai yatakaa pale mpaka yatakapo anguliwa...
Pia kuna chumba cha ziada ambacho ndani ya chumba hichi hukaa viumbe ambao hapo baadae ikatokea malkia amekufa au mfalme atachukuliwa mmoja wao na kulishwa vizuri na baadae kushika nafasi ya malkia au mfalme...
Ndani ya Kichuguu huishi viumbe wajulikanao kama Mchwa ambao ndiyo wakazi sana sana ingawa waweza kukuta kichuguu kinamilikiwa na viumbe wengine ingawa wajenzi hasa wa kichuguu ni mchwa....
Bila mchwa hakuna kichuguu....Mchwa ni wadudu wadogo wadogo ambao wamejigawa katika makundi manne...Kundi la Kwanza ni Malikia na Mfalme(King&Queen)
             Kundi la Pili ni Walinzi(Solders)
             Kundi la Tatu ni Wafanyakazi(Workers) na kundi la 4 hujulikana kama Aletes
Kazi kubwa ya Malkia na Mfalme ni kuzalisha tu
Na walinzi kazi yao ni kuhakikisha kuwa kichuguu kina usalama muda wote ambao nao wamegawana majukumu kuwa walinzi wachache wabaki ndani kumlinda Malkia wao pamoja na Mfalme na walindi wengine waangalie usalama wa nje na lango la kuingilia ndani ya kichuguu.Kwa kawaida walinzi hawana macho na huwasiliana kwa kugonganisha vichwa au kugonga vichwa vyao kwenye kuta za ndani ya kichuguu....
Kwa upande wa Wafanyakazi,kazi yao kubwa ni kulisha familia nzima kwenye kichuguu,wakianzia kuwalisha malkia na mfalme,walinzi na Aletes,kazi nyingine kubwa walio nayo wafanyakazi ni kutengeneza kichuguu pindi kinapoharibiwa labda na mvua,mnyama ama binadamu,pia wafanyakazi wanao kazi kubwa sana ya kumpooza malkia pindi joto linapoongezeka na wafanyakazi wanauwezo wa kwenda umbali wa mita 100 kutafuta maji kwa ajili ya kumpooza malkia kwa sababu mwili wa malkia umejaa mafuta....
Wafanyakazi pia huwalisha Aletes na hutoka nje ya kichuguu kwa ajili ya kukusanya majani kwa ajili ya kutengeneza chakula cha kutosha na kuchanganya na mchanganyiko maalum ili kutengeneza Royal Jelly kwa ajili ya malikia na Aletes kwa ajili ya kuandaliwa kuwa malkia wa baadae kama itatokea malkia atakufa......

JE UNAJUA KUMBI-KUMBI NI NINI au WANATOKA WAPI?
Kumbi-kumbi ndiyo tunao waita Aletes ambao mwanzo walikuwa wanalishwa na mchwa Wafanyakazi,hivyo baada ya kukomaa hutoka ndani ya kichuguu na kwenda kutafuta sehemu ya kwenda kutafuta sehemu ya kwenda kuanzisha kichuguu chao na kwa kawaida jike huwa nyuma mama mbele na mbawa walizokuwa nazo ni za mda tu kwa ajili ya kutafuta pahala pa kuanzisha kichuguu chao na wakishapata sehemu hiyo hufukua kiasi na kuchichimbia humo....Kwa kawaida huwa hawali kitu chuchote kwa sababu mwanzo walikuwa wameshajikusanyia chakula chao cha kutosha na wataishi bila kula mpaka mpaka jike litakapo anza kutoa mayai na pindi mayai yatakapoanguliwa wale watoto ndiyo watakuwa wafanyakazi wao na kuanza kugaiwa majukumu ili kukiendeleza kichuguu......na adui yake mkubwa ni wewe mlaji wa kumbikumbi.so kwa wale mnaokula kumbikumbi msione ana-mafuta ukamtamani mwche atafute life bhanaaaaaaaa........mwacheeeeeee
                                                               Asanteeeeeeeeee

Monday, July 8, 2013

Ifahamu japo kidogo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti...

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilianzishwa mwaka 1951 ikiwa na ukubwa wa takribani kilomita za mraba 14,763...ni Hifadhi ya kwanza kutangazwa kama hifadhi ya Taifa
Hifadhi hii inasikfika kwa kuwa na makundi makubwa ya wanyama kama vile NYUMBU,SWALA GRANTI,SWALA TOMI,TEMBO,SWALA PALA,MUHANGA,NYANI,MBWHA MASIKIO,CHUI,DUMA,TWIGA,SIMBA,CHOROA,MONDO,PUNDA MILIA,KIBOKO,MBWA-MWITU,MYEGERE na ndege wa aina zaidi ya 500 hasa makundi makubwa ya MBUNI hupatikana katika hifafadhi hii.
Hifadhi hii inasifika pia kwa wanyama wahamao kutoka sehemu moja hadi nyingine kutafuta malisho mazuri na huhama kuanzia Serengeti Tanzania kwenda mpaka pori la akiba la Masai Mara na kurudi tena Tanzania kupitia Ngorongoro kwenda tena Serengeti....Hii hufanya tena kuwa ajabu lingine katika hifadhi hii.....
Serengeti pia husifika kwa kuwa na mawe makubwa ambayo nayo yamekuwa kivutio kikubwa kwa watalii.....lakini kivutio kikubwa ambacho ni kivutyio kikubwa katika hifadhi hii ni...
KUHAMA KWA NYUMBU KUTOKA SERENGETI-Tanzania kutoka kusimi mwa hifadhi kwenda kaskazini mwa hifadhi na kurudi tena kusini mwa hifadhi kupitia  MASAI MARA inchini Kenya na Kurudi tena Tanzania ambapo NYUMBU wapatao Millioni Moja na Nusu wakiambatana na PUNDA MILIA wapatao 600,000 na SWALA TOMI zaidi ya 300,000 ambapo wanyama walao nyama kama vile SIMBA,DUMA,CHUI na wengineo huambatana nao kwa sababu katika safari yao wapo nyumbu wanao zaliwa na wapo wanao umia na wanaoumwa pia...
Mamba pia hujipatia chakula chao kupitia kwa hawa wanyama pia wanaohama kwani katika kuhama kwa wanyama hawa hukatisha katika mito mbali mbali kwa mfano mto grumeti n.k
Viumbe wapya wa Nyumbu huzaliwa takribani 3000 kwa siku....

Mda mzuri wa kuitembelea hifadhi hii ili kuona KUHAMA kwa NYUMBU ni kuanzia mwezi wa Kumi na mbili mpaka wa 7 kwa ajili ya kuona NYUMBU wanavyohama na mwezi wa 6 mpaka wa 10 kwa ajili ya kuona wanyama wanaowinda....

Katika hifadhi hii yenye maajabu inayo huduma nyingi za kimalazi ambazo zipo ndani na nje ya hifadhi kwa mfano,Sengeti Serena,Sopa Lodge,Huka,Grumeti River Camp,Serena Kirawira n.k.....
....Kufikika kwake ni kwa njia rahisi kwani waweza fika kwa gari hata kwa ndege na nikama kilometa 335 kutoka jijini Arusha



                                                                    KARIBU

Sunday, July 7, 2013

GIVE UP....





Give up your need to always be right. There are so many of us who can't 

stand the idea of being wrong wanting to always be right even at the risk of 

ending great relationships or causing a great deal of stress and pain for us 

and for others. It's just not worth it. Whenever you feel the 'urgent' need to 

jump into a fight over who is right and who is wrong, ask yourself this 

question : Would I rather be right, or would I rather be kind?'

What difference will that make? Is your ego really that big? 

Natamani tuendelee kua na Amani na Upendo kama wao...

Ni kweli kabisa amani na upendo kwetu sie binadamu vimepungua sana , Inafikia wakati sisi kwa sisi tunashindwa kusaidina katika matatizo mbalimbali hata kama mtu anauwezo wa kufanya hivo ilimradi tu yeye aone mwenzake anadhalilika, zaraulika, taabika n.k. Hii yote ni kwa sababu ya Ubinafsi ama Chuki binasfi--Si vizuri kumdharau mtu au kumtakia mabaya kwani LEO KWAKE KESHO YAWEZA KUA KWAKO japokua huo mzunguko si mzuri pia. Hebu tumone Mnyama Twiga ambaye kiukweli unaweza sema ni mnyama wa kuigwa kama tungeweza kuishi kama wanyama...

TWIGA (GIRAFFE)

Huyu ni mnyama ambaye maisha yake siku zote ni ya amani na upendo kwa upole wake alonao, utamuona katika mazingira yake ya kujidai (porini) akitembea kwa madaha huku akiyumbisha shingo yake ndeeeeefu na ndo mnyama pekee ambaye anatumia aina pekee ya kutembea inayoitwa AMBLING STYLE inamaanisha kutembea kwa kunyanyua mguu na mkono wa upande mmoja kisha kufatiwa na upande mwingine. Kwa haraka haraka mnyama huyu pia huonesha upendo zaidi pale anapo toa MSAADA kwa mwenzake kwa kumkuna kitendo kinachoitwa GROOMING. Angalia picha hii......Inapendeza kwa kweli kwa kuonesha jinsi gani Upendo umetawala kwa wanyama kwani Twiga ni mfano tu lakini wapo wanyama wengine pia
wenyetabia nzuri kama hizo. Hebu na sisi binaadamu tubadilike jaman.....

Scientific Name: Giraffa Camelopardas
Sex difference: Female smaller about 4.9 meters than Male (about 5.5 meters)

Saturday, July 6, 2013

Ubinadadamu kazi....

Nakuambia nimefanikiwa unachukia,nilipokuwa sijafanikiwa tulikuwa marafiki sasa mafanikio yangu yamekuwa kikwazo kwako....oooohh my friend.....why???.Tenda wema usepe zako usingoje shukurani.....

Kweli ubinadamu kazi ingawa hatulipwi mishahara.....

Janga kwa mwananchi wa Kawaida....

Hiii ni HAKI au JANGA????

Hii ni Hakiiiiiiii????

Tozo ya shilingi 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu Unayomiliki....majanga haya....Je watu wa vijijini wenye vipato vya chini itakuwaje?na ndiyo uchumi unakua au unashuka?.Watu wataanza kutumia laini moja ya simu sasa....na je ni nani anaye stahili kulipa gharama hizooooo?mteja au kampuni husika....oooooh buku....daaaa buku....wapitunapelekwa Watanzania?????Laini umetengeneza wewe nilipe mie hayo si majanga jamani?????Hebu serekali tusaidieni jamani,sisi ni wenzenu pia.......

Hiii ni HAKI au JANGA????

Hii ni Hakiiiiiiii????

Tozo ya shilingi 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu inayomiliki....majanga haya....Je watu wa vijijini wenye vipato vya chini itakuwaje?na ndiyo uchumi unakua au unashuka?.Watu wataanza kutumia laini moja ya simu sasa....na je ni nani anaye stahili kulipa gharama hizooooo?mteja au kampuni husika....oooooh buku....daaaa buku....wapitunapelekwa Watanzania?????Laini umetengeneza wewe nilipe mie hayo si majanga jamani?????Hebu serekali tusaidieni jamani,sisi ni wenzenu pia.......

Friday, July 5, 2013

Hili nalo nenooooooooooooo.......

Hili nalo nenoooooooooooo..........



Hata mwaume uwe bahili kiasi gani huwezi kumpa mwanamke mimba nusu...

Haha kalale nachoo....kidalipoooo...

Je wamjua Simba-mangu?


Simba-mangu(Caracal) ni mnyama mzito mwenye uzito zaidi kati ya jamii yake ya mapaka,Simba mangu dume anaweza kuwa na uzito kati ya  kilo 15 mpaka 18 na majike uzito wao ni kati ya Kilo 13 na kuendelea........
Miguu ya nyuma ya Simba mangu ni mirefu kuliko ya mbele ya mbele...Simba mangu ana uwezo wa kuona zaidi usiku na hata mchana tofauti na wanyama wengine wanaoweza kuona vizuri zaidi usiku au wanao-ona vizuri mchana lakini usiku hawaoni vizuri,Simba-mangu yeye usiku na mchana anaona vizuri tu...
Simba mangu huwa wana-aibu na niwapandaji wazuri wa miti.

Hupenda Kula nini?

Simba-mangu hupendelea kula vitu kama vile,Pimbi mawe(Hyrax),Mbuzi mawe(Klipsringer),panya,Sungura,Mijusi,na Ndege...na wanauwezo wa kuruka juu hadi futi 11 sawa na mita 3-4....

Hukaa na mimba mda GANI?

Huwachukua takribani siku 62-82 sawa na miezi miwili na zaidi na watoto kati ya 2-4 huzaliwa na wanaweza kuishi hadi miaka 12...

MAADUI:

Wanyama wakubwa kunzidi yeye mfano,chui,simba n.k



Thursday, July 4, 2013

Je wamjua Mnyama anayemiliki majike Mengi?

Swala Pala ni mnyma mwenye mashabiki wengi sana porini,hupendwa na watalii sana..Hupendelea kutembea kwa makundi makubwa makubwa kati ya swala 15-20 na katika kundi hili wapo mabachela na mabinti wadogo wadogo na dume moja.Dume ndiye anayeliongoza kundi zima na kulimiliki kundi hilo na kuna wakati dume hupoteza uzito kwa kuwa-busy kulilinda kundi lake dhidi ya maadui wengine na pia uzito hupungua kwa sababu ya kujamiana na wakeze,hivyo hutumia mda mwingi sana kwenye kujamiana na kuangalia familia yake kuliko kula...Dume peke yake ndiye mwenye PEMBE......
Swala hupendele kula nyasi fupi,matawi ya miti na hupendelea sana kunywa maji lakini anaweza kukaa mda mrefu bila kunywa maji..........
Swala hubeba mimba kwa takribani miezi 6 au 7 na mtoto mmoja tu ndiye huzaliwa na swala huweza kuishi mpaka miaka 14 au 15 na maadui zao wakubwa ni BINADAMU,CHUI,DUMA,SIMBA ingawa si Sanaa pamoja na M'bwa Mwitu

Wednesday, July 3, 2013

Je wayajua maajabu ya Mbuyu?

Historia inatueleza kwamba hapo zamani mbuyu ulimuudhi mwenyezi Mungu na kutupwa duniani juu chini...Mti huu husemekana kuwa waweza kuishi maelfu ya miaka na miaka,kwa makadirio waweza kuishi hata miaka 3000...
Mti huu hutumiwa na binadamu kwa matunda yake na hata wanyama wa porini hasa Tembo huutumia mti huu wakati wa kiangazi kujipatia maji kupitia kwenye magome ya mti huu .Nyani na Tumbili nao hawapo nyuma katika kuutumia mti huu kujipatia kiburudisho cha matunda ya mbuyu..Ubuyu ambao pia unatokana na mbuyu hutumika kutengenezea sabuni za kuogea n.k n.k..
Unga unga wa ubuyu hutengeneza pia juice,pia kwa upande mwingine tunda la Mbuyu hutumika kwa mapambo mbalimbali....
Katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire upo mbuyu{Pochers Hide} ambao ulitumiwa majangili kujihifadhi baada ya kuwinda wanyama kinyume na sheria...Mbuyu huu ulitumika kama nyumba kwani kuliishi familia nzima ingawa ulikuwa ndani ya hifadhi ya Tarangire.Ndani ya mbuyu huu kuliwekwa kitanda na vitu vingine vya matumizi ya ndani...Lakini kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho kwani wahusika waliweza kushughulikiwa na kuuacha Mbuyu huwa kuwa historia ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire...Tazama picha hapo juu....
                                               

Monday, July 1, 2013

Je Wamjua Vizuri mnyama anayeitwa NYEGERE?

Je wamjua Mnyama wa Pili kwa Ukubwa Duniani?

Tembo{Loxodonta Africana}ni mnyama wa pili kwa ukubwa duniani ambaye anakadiriwa kuwa na kilo zaidi ya 7000 sawa na Tani 7 au hata Tani 8 sawa na kilo 8000 na kwa kawaida dume huwa mkubwa kuliko tembo jike...
Tembo ambaye ni wa pili kwa ukubwa baada ya NYANGUMI ni miongoni mwa wanyama wanao-ongozwa kwa kuwindwa sana na majangili kwa kile kinachodaiwa kwamba meno yake kuwa na thamani kubwa sana....
JE HUPENDELEA KULA NINI?
-Tembo hupendelea kula mchanganyiko wa vyakula mbali-mbali ambavyo hujumuisha Magome ya miti,Mizizi,Matunda,Nyasi,Majani Machanga n.k...Pia hupendelea kula migomba,maboga,miwa na hata mahindi na chumvi.Kwa siku hula mpaka kilo 150-300 za chakula na hunya maji mara mbili kwa siku.....Ulaji wake wa vyakula mchanganyiko ndiyo unaompa kinga mwilini kwani baadhi ya nyasi na matunda anayokula miongoni mwake ni dawa hivyo kumfanya awe mnyama anayeishi miaka mingi tofauti na wanyama wengine....Tembo huweza kuishi mpaka miaka 70...
JINSI WANAVYOISHI
Huishi kwa makundi makubwa makubwa na kwa tembo ambaye ni mgonjwa au mzee hutengwa na familia...
KUZAA KWAO..
Huchukua miezi 22-24 sawa na Miaka miwili na zaidi na daima huzaliwa mtoto mmoja tu na hukadiriwa kuwa na uzito zaidi ya 200
ADUI .
Binadamu na magonjwa

welcome to spider blog

welcome to spider blog